Baada ya kipande cha video kusambaa mitandaoni
kikionyesha mwanafunzi aliyekuwa akiadhibiwa kwa kushambuliwa na walimu, Waziri
wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameitoa taarifa kupitia ukurasa wake
wa Instagram ambapo ameandika hivi
Mnamo Tarehe 28.9.2016,
mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie
Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke
Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.
Mwl Frank alitoa assignment ya
Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya,
darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga
wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza
kumpiga vile.
Tangu tar 29. September
mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa
akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo
wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao.
POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi
aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar
wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi
huyo.
No comments:
Post a Comment