Kim Kardashian aliingiwa na hofu kubwa baada ya kuvamiwa
na majambazi jijini Paris Ufaransa. Mwanamitindo huyo alitekwa kwa muda na
kuwaomba majambazi wasi mtoe uhai wake. Baada ya kusalimika , ilimbidi abadili
mfumo wake wa kutumia mitandao ya kijamii kama alivyo amini ndio sababu ya yeye
kuvamiwa.
Maafisa wa Paris waliamini mitandao ya kijamii imepelekea
yeye kupatikana kirahisi. Umaarufu wake haufai kuonesha kilakitu alichonacho na
wapi anakwenda. Ni hatari sana anapotumia mtandao wa Snapchat kuonesha kila
sehemu anazokuwepo ni hatari sana kwa usalama wake. Kim aliongeza kuwa
mashabiki wake wamemuambia mitandao ya kijamii imechangia kiasi kikubwa katika
kuvamiwa kwake. Kwa mujibu wa TMZ, Kim kujipa likizo ya mwezi mmoja. Wakati
akirudi kazini hato onesha tena vitu vyake , pia matukio yake ya mitindo atakua
akionesha kwenye mitandao ya kijamii kwa uchache, tofauti na hapo mwanzooni.
Yeye binafsi alisema "vitu havina maana yoyote. Siyo
kwamba pesa ndio kila kitu, "akiongeza," Siyo thamani yake. Maskini
Kimmy. Hakuna mtu anastahili kupitia majanga aliyeyapata , hakika, kusitisha
kuposti vitu vya thamani kwenye mitandao ya kijamii itasaidia kuweka mambo yake
binafsi na kuzuia mtu yeyote ambaye anataka kusababisha madhara kwake. By
Mhariri Betz.
Usipitweee!
ReplyDelete