Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Malaika ambaye kwa sasa
anafanya vizuri na wimbo wake 'Rarua' amefunguka na kusema kuwa watu wanapokuwa
wakitumia picha zake au wakiandika mambo yanayohusu maisha yake binafsi ni kitu
ambacho kinamuumiza sana.
Malaika alisema hayo kupitia kipindi cha 'Ngaz Kwa Ngaz'
kinachorushwa na EATV na kudai kuwa muda mwingine huwa anaudhika na kukasirika
pindi anapoona watu wanachangia kwenye mitandao ya kijamii na kuhusisha mambo
yake ya kimuziki pamoja na mambo yake ya kifamilia.
"Ninapokuwa
napost picha kwenye mitandao ya jamii wakati mwingine napata 'Comments'
mbalimbali nyingine zinakuwa zinaudhi, hasa pale mtu anapo kuja kuandika na
kuhusisha maisha yangu ya muziki na maisha ya familia yangu ni kitu ambacho
huwa kinaniumiza sana, na ni kitu ambacho sikipendi kwa sababu unapokuwa
unanichukulia mimi kama msanii unatakiwa unichukulie mimi kama mimi. Na kama
una jambo lolote unataka kuniambia niambie mimi kama mimi lakini huwezi ku
'involve' mambo yangu ya muziki na mambo yangu ya familia yanaumiza sana"
alisema Malaika.
No comments:
Post a Comment