Kampuni ya Vinywaji Baridi ya CocaCola, imejitokeza
kuiunga mkono EATV LTD kwenye Tuzo za EATV (EATV AWARDS), ili kuinua sanaa ya
Afrika Mashariki.
Afisa Masoko Msaidizi wa CocaCola,Pamela Lugenge (Kulia) akiwa na
Meneja Mauzo na Masoko wa EATV LTD, Roy Mbowe. |
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Pamela
Lugenge ambaye ni Afisa Masoko Msaidizi wa CocaCola, amesema wao kama kampuni
inayojihusisha na kuinua vipaji kwa vijana, hawakuwa na sababu ya kutounga
mkono jambo hilo ambalo ni muhimu na kubwa kwa wasanii wetu, ambao ni mifano
bora kwa vijana.
“Kama
mnavyojua tuna sababu milioni za kujiamini, kampeni ambayo inahamasisha watu
kujiamini katika vipaji vyao na waendelee kuvipigania na kama Copa CocaCola
ambayo ni football tournaments, inayovumbua vipaji vya vijana hapa Tanzania”,
alisema Pamela
Pamela
aliendelea kusema ….................”So, fursa kama hii ya East Africa TV
ambayo inawatambua wasanii wetu wa Tanzania na kuwashukuru, kwa vipaji vyao na
kuwa role model kwa vijana , sisi hatukuweza kutoshiriki, na kwa kampeni yetu
ya mwaka huu ambayo ni onja msisimko, tukaona ni vizuri wakati tunaangalia
#EATVAwards, basi tuwe tunajiburudisha na vinywaji vya CocaCola”.
Kampuni
ya CocaCoala imekuwa ikiunga mkono mambo mengi ya kuinua vipaji kwa vijana,
ikiwemo na mashindano makubwa ya kucheza ya Dancee 100%, ambayo pia
yanaendeshwa na EATV LTD.
No comments:
Post a Comment