Samsung imelazimika kusitisha utengenezaji wa
simu za Galaxy Note 7 kutokana na tatizo lake la kulipuka.
Kufuatia tangazo hilo, hisa zake zilishuka kwa asilimia 8, na kupunguza dola milioni 17 za thamani yake sokoni.
Simu hiyo ilipangwa kuwa mshindani wa iPhone 7, lakini badala yake imekuja kuharibu vikali heshima ya Samsung. Wachambuzi wanadai kuwa uamuzi wa Samsung kuipiga chini Note 7 moja kwa moja – itasababisha hasara ya dola bilioni 9.5 za mauzo na kupoteza faida ya dola bilioni 5 za faida.
Kwenye maelezo yake ya mwanzo, Samsung ilisema itayaomba makampuni na mawakala wake dunini kote kuacha mauzo ya Galaxy Note 7, wakati inachunguza chanzo cha kushika moto. Iliwaomba pia wateja wenye simu za awali za Galaxy Note 7 au zile walizobadilishiwa, kuzizima na kuacha kuzitumia kabisa.
No comments:
Post a Comment